Jumuiya ya waislamu nchini Nigeria katika jimbo la Kaduna imepanga kuwafanyia harusi ya pamoja watu waliosilimu kuanza maisha yao mapya na kujenga familia imara.
Harusi hiyo ya pamoja itakuwa na maharusi wapatao 50 na ni baada ya watu hao waliosilimu kupata mafunzo na elimu ya misingi ya dini kwa muda wa miezi mitatu.
Mratibu wa zoezi hilo Sheikh Ahmad Gumi alisema wanawafanyia jambo la ndoa ili waepukane na tabia mbaya na waone uzuri wa uislamu.
"Kama watu wakati mwingine wanakabiliwa na upweke baada ya kupoteza wake zao ambao hawakuweza kukubali kusilimu", alisema Sheikh Gumi.
Sheikh aliongeza kusema kuwa kabla ya kufunga ndoa maharusi wote watapimwa damu zao kwa ajili ya kuangalia kama wameathirika au la.
Hii ni mara ya nane kwa kundi la watu 50 waliosilimu kumaliza mafunzo ya dini kwa muda wa miezi mitatu.
