Rais Samba-Panza amesema waasi hao, wamepoteza mwelekeo na hawana dhamira yoyote. Amesema wapiganaji hao ambao walikuwa watetezi wa jamii, wamegeuka na kuwa wauaji na waporaji.
Maelfu ya Waislamu wameukimbia mji huo na kukimbilia nchi jirani ya Cameroon.
Jamhuri ya Afrika ya Kati imetumbukia kwenye machafuko ya umwagaji damu ambapo Wakristo wanawashambulia na kuwaua Waislamu tangu mwaka uliopita.
![]() |
| Catherine Samba Panza |
