Sheikh Omar ambaye ni khatwibu wa Msikiti wa kichangani uliopo Magomeni, jijini Dar es Salaam alitoa ujumbe huo kuwaendea Waislamu wote nchini kwa Audio aliyoisambaza kwa njia ya Whatsapp.
"kazi kubwa ni kupambana na vitu mbalimbali vinayvotiwa katika jamii za kiislamu na waislamu kwa kutokufahamu kwao wanaviiga, ni makosa makubwa sana", alisema
Akitolea mfano mambo ambayo waislamu wamekuwa wakiiga bila ya kujua asili yake ni siku ya valentine Day. Alisema waislamu katika siku hiyo wanapeana zawadi za maua mekundu, wanavaa nguo nyekundu bila ya kuelewa asili ya sikukuu hiyo.
Aliongeza kusema kufanya hivyo ni makosa makubwa sana katika uislamu kwani upendo hauoneshwi kwa siku moja bali kwa siku zote.
"Ndugu zangu tuipige vita siku hii,tuipige vita sherehe hii na Mwenyezi Mungu atatulipa kwa sababu ni sehemu ya jihadi kwa upande wetu", alimaliza Sheikh Alhad.
Sikukuu ya Valentine Day huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka. Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma ambapo alikuwapo padri Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo.
Inasemekana kwamba Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera).
Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari. Valentinus alipinga jambo hili hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa. Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine "kupiga naye stori". Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.
Kwamba muda mchache kabla hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake ya kuaga akiweka sahihi "From Your Valentine" (kutoka kwa Valentine wako). Valentine akanyongwa tarehe 14 februari mwaka 269 AD.
Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia wanawake waliowapenda salamu za mapenzi. Mwisho wa barua walihitimisha kwa maneno haya, Kutoka kwa Valentinus wako.
| Sheikh Omar Alhad Omar |