Mahakama ya Kenya siku ya Jumatano jana ilifuta mashtaka dhidi ya watu 41 waliokamatwa mapema mwezi huu wakati wa uvamizi katika Masjid Mussa na kuwaachia wengine 29 kwa dhamana, AFP iliripoti.
Polisi walivamia masjid Mussa tarehe 2 Februari, wakiwakamata washukiwa 129 wanaotuhumiwa kuhudhuria mkutano wa msimamo mkali, kuchochea vurugu kubwa katika mji wa bandari.
Washukiwa kimsingi wote walishtakiwa kwa kuwa wanachama wa Al-Shabaab, pamoja na mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na kuwa na silaha za moto na kuchochea vurugu.
Tarehe 11 Februari serikali iliwaachia watuhumiwa 33 na kuwashtaki rasmi watu 70 siku moja baadaye katika makosa saba, ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa kikundi cha wanamgambo wa Al-Shabaab.
Hakimu Richard Oden-yo siku ya Jumatano aliagiza watu 41 kati ya hao walioshitakiwa kuachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi. Washukiwa 29 waliobakia waliachiwa huru kwa dhamana ya shilingi 500,000 ya kenya kila mmoja.
