"Sisi hatuhimizi uvaaji wa Hijab kwa siku moja bali tutaendelea kuwahimiza wanawake umuhimu wa kuvaa Hijabu kwa siku zote", alisema kiongozi wa wanawake katika chama cha Jamat -el- Islam, Farhana Aurungzeb.
Aidha chama hicho kiliandaa mikutano, semina na kusambaza mitandio katika taasisi za elimu na ofisi kadhaa.
"Kauli mbiu yetu ya mwaka huu ni Hijabu ni chaguo langu, ni fahari yangu ( hijab- my choice, my pride). kauli hii huonesha kwamba kwetu kuvaa Hijabu ni wajibu kwa mwanamke wa kiislamu", alisema Farhana Aurungzeb
ambaye aliwahi kuwa mwakilishi mwanamke katika halmashauri ya manispaa ya karachi mwaka 2002 mpaka 2005.
hijab Day imeadhimishwa takribani nchi 116 duniani kote na waislamu na wasio waislamu. Huu ni mwaka wa pili tangu kuanzishwa siku ya Hijabu dunia (World Hijab day) Kwa mara ya kwanza ilianzishwa mwaka 2013 na mwanamama Nazma Khan mkazi wa New York, Marekani ili kuhamasisha wanawake waislamu na wasio waislamu kuvaa Hijabu.
Lengo ni kuweka jitihada za kuendeleza uelewa wa uvaaji wa Hijabu na kuweka taarifa sawa kwa wale wanapotosha kuhusu Hijabu. Hijabu imekuwa ikitafsiriwa ni ishara ya ukandamizaji na ubaguzi kwa mwanamke.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la kupinga Hijabu katika nchi za Magharibi hasa nchini Ufaransa ambapo vazi hilo la Kiislamu limepigwa marufuku katika baadhi ya maeneo ya umma.
![]() |
| Wanawake wa Pakistan |
