Wengi wa waandamanaji hao walikuwa ni wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari na walibeba mabango kadhaa yenye ujumbe wa kuonesha uhalali wa wao kuruhusiwa kuvaa hijabu wakiwa shuleni.
Maandamano hayo yalifanyika katika kuadhimisha siku ya Hijabu dunia. Akizungumza na vyombo vya habari Amirah wa wanafunzi wa kiislamu alisema ikiwa madai yao yatapuuzwa watapiga hatua nyingine ya kwenda mahakamani kudai haki yao kisheria.
Nae gavana wa jimbo la Lagos, Babatunde Fashola alisema shule za umma hazina budi kuruhusu wanafunzi wa kiislamu wavae Hijabu.
Alisema ikiwa watakaidi basi watawaunganisha wanafunzi wote wa kiislamu kuipinga serikali na kuitangaza kama adui kwa jamii ya kiislamu.
Aliongeza kusema ikiwa kama jamii ya kiislamu ni sehemu ya walipa kodi basi shule hizo za umma ziruhusu wanafunzi kuvaa Hijabu.
![]() |
| Wanafunzi wakiandamana Mjini Lagos |
