Sunai Phasuk mwakilishi wa HRW nchini Thailand amesema kuwa, shirika hilo linataka ufanyike uchunguzi wa kina ili kubaini hatima ya Waislamu hao ambao hadi leo hawajulikani walipo.
Hayo yamejiri baada ya serikali ya Thailand kutangaza kuwa, wakimbizi hao wa Rohingya waliondoka kwenye makambi waliyokuwa wakihifadhiwa yapata miezi mitatu iliyopita na kurejea kwenye jimbo lao la Rakhine nchini Myanmar.
Waislamu hao walilazimika kukimbilia nchini Thailand baada ya kushadidi vitendo vya ukatili na mauaji vinavyofanywa na Mabudha dhidi ya Waislamu nchini Myanmar.
Mwakilishi wa Human Rights Watch amesema kuwa kitendo cha kuwafukuza Waislamu kutoka nchini mwao ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa, na kusisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni marufuku kuwarejesha wakimbizi katika eneo linalohatarisha usalama na maisha yao.
Waislamu wanaunda asilimia 5 kati ya watu milioni 60 nchini Myanmar, lakini wamekuwa wakikandamizwa, kuteswa na kuuawa tokea nchi hiyo ijipatie uhuru mwaka 1948.
| wakiwa katika makambi ya wakimbizi |