UNICEF inasema wiki za karibuni zimeshuhudia viwango vya juu vya kupindukia vya ukatili dhidi ya watoto wakati huu ambapo kuna mashambulio ya kulipiza visasi yanayofanywa na kikundi cha waasi cha Ant-Balaka.
Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Afrika Magharibi na Kati Manuel Fontaine amekariri akisema kuwa ongezeko la ghasia kwenye mji mkuu Bangui na kwingineko watoto wanazidi kuwa walengwa kwa misingi ya dini zao au jamii wanazotoka. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF Geneva.
Katika miezi miwili iliyopita UNICEF imethibitisha kuuawa kwa watoto 37 na kujeruhiwa kwa wengine 97, na baadhi ya matukio haya yalifanyika kwa ukatili ambao huwezi kuelewa. Katika muda huo pia UNICEF na wadau wamepokea taarifa za matukio 197 ya ukatili wa kingono kwenye kambi za wakimbizi wa ndani mjini Bangui, visa 27 kati ya hivyo ni dhidi ya watoto.
UNICEF inatoa wito kwa serikali na jamii, viongozi wa dini na vikundi vya kiraia ambao wamepatiwa dhamana ya uongozi kusaidia kumaliza ghasia na kuondoa jamii zao kwenye mazingira hayo ambamo watu wazima wanakiuka haki za watoto.
UNICEF imetaka watekelezaji wa vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto wachunguzwe, washtakiwe na waadhibiwe.
![]() |
| Binti huyu ni mmoja wa wahamga |
