Akizungumza mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon amesisitiza kuwa, jamii ya kimataifa inapasa kuchukua hatua za haraka za kuzuia wimbi la jinai mpya na maangamizi makubwa ya kidini na kikabila nchini humo.
Ban Ki moon amesisitiza kwa kusema, "wingu zito jeusi la jinai kubwa na maangamizi ya kidini na kikabila limetanda katika anga ya Afrika ya Kati".
Ban Ki moon ameongeza kuwa, iwapo mgogoro wa hivi sasa unaoendelea kutokota Jamhuri ya Afrika ya Kati hautakomeshwa, bila shaka kuna wasiwasi nchi hiyo itaendelea kushuhudia mapigano hadi miongo kadhaa ijayo.
Hivi karibuni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International lilikosoa kimya cha jamii ya kimataifa kuhusiana na mauaji yanayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa ya shirika hilo la kimataifa ilieleza kuwa, lina ushahidi wa kutosha unaoonyesha ukatili na mauaji yanayofanywa na kundi la Kikristo la Anti Balaka dhidi ya maelfu ya Waislamu nchini humo.
![]() |
| Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki moon |
