Tuesday, 11 February 2014

SHEIKH SUDAIS AKAGUA UKARABATI WA MSIKITI MTAKATIFU WA MAKKAH

Mkuu wa urais wa Misikiti miwili mitakatifu Sheikh Abdul Rahman ibn Abd al-Aziz Al- Sudais عبد الرحمن السديس 
jumapili amekagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa makkah kwa ajili ya upanuzi wa 'mataf' eneo linalozunguka kaaba takatifu.

Akizungumza na waandishi wa habari, alisema ziara ilikuwa na lengo la kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati
kwa kuzingatia usalama na viwango vya ubora. Sheikh Sudais aliambatana na naibu wake Sheikh Mohammed Al-Khozaim.

Naibu Mwenyekiti wa kampuni ya Binladin Group, Yahya Binladin ndiye aliyempokea Sheikh Sudais na kumtembeza sehemu za ujenzi.Kampuni ya Binladin Group ndiyo inayojenga msikiti huo. 

Aidha, Sheikh Sudais alimshukuru msimamizi wa misikiti miwili Mitakatifu Mfalme Abdullah kwa ajili ya kuanzisha mradi wa upanuzi wa mataf ambao utaongeza uwezo wake kutoka watu 40,000 mpaka 130,000 kwa saa.


Sheikh Sudais katikati akikagua upanuzi wa mataf