Bw. Obama alikuwa akizungumza Alhamis wakati wa dhifa ya kila mwaka ya maombi ya kitaifa jijini Washington, ambako alisema yeyote anayemdhuru mwingine kwa kutumia imani ya dini anadhulumu uhusiano wake mwenyewe na Mwenyezi Mungu.
Aliwasihi walioshiriki katika mamombi hayo kuwaombea wote waliokamatwa na kuzuiliwa kutokana na imani zao za kidini, akiwemo Kenneth Bae aliyezuiliwa Korea Kaskazini na Saeed Abedini aliyezuiliwa huko Iran.
Maombi ya kitaifa ya kila mwaka huandaliwa na wabunge wa Marekani katika majengo ya bunge. Na kila rais wa Marekani amehudhuria maombi hayo tangu yalipoanza mwaka wa 1953.
Januari 22, mwaka huu taarifa kutoka makao makuu ya jeshi la marekani ilitoa ruhusa kwa askari wake kuvaa mavazi ya dini kama ishara ya kuheshimu imani za dini zote.
Aidha mwanajeshi ataruhusiwa kuvaa hijabu akiwa katika sare za kijeshi.
![]() |
| Rais Barack Obama na mkewe Michelle katika maombi ya kitaifa, Washington Feb 6, 2014 |
