Imeelezwa kuwa, Rais Mujica Cordano ametetea uamuzi wake wa kuruhusu kisheria utumiaji bangi nchini Uruguay na kuutaja kuwa ni 'wenzo kwa ajili ya amani na maelewano' na kwamba unapaswa kupongezwa.
Taasisi ya Amani ya Mihadarati imethibitisha kwamba, Rais Cordano ni miongoni mwa wanaopendekezwa kutunukiwa tuzo ya amani na Nobel.
Mnamo mwaka 2012 taasisi hiyo iliunga mkono mpango wa Rais wa Uruguay kuruhusu dawa hizo za kulevya na kusema ni moja ya masuala ya haki za binadamu.
Mwezi Disemba, 2013 serikali ya Uruguay ilipitisha sheria ya uhuru wa kutumia bangi, jambo lililosababisha nchi hiyo kukabiliwa na ukosoaji mkubwa wa jamii ya kimataifa.
Uruguay inahesabiwa kuwa nchi pekee duniani ambayo imeruhusu rasmi matumizi ya bangi. Sheria hiyo ya kuruhusu matumizi ya bangi itaanza kutekelezwa rasmi mwezi Aprili mwaka huu.
Upitishwaji wa sheria za namna hii ni kiashiria cha upotofu pindi mwanaadamu anapokosa muongozo wa dini hususani uislamu.
![]() |
| Jose Alberto Mujica Cordano |
