Thursday, 6 February 2014

MBUNGE: KITENDO CHA POLISI KUUA WAISLAMU NA KUWAPIGA MSIKITINI NI UGAIDI

Mwanasiasa Maarufu na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nasir ameikemea vikali hatua na kitendo cha Wanajeshi kwa kushirikiana na Polisi kuwaua waislamu na kukiita kitendo hicho kuwa ni cha Kigaidi na kisichokubalika.

"Msimamo wangu mimi kitendo kilichofanywa na Wanajeshi na Polisi ni kitendo tunachoweza kukifafanua kuwa ni kitendo cha Kigaidi hamna kitu kingine", alisema na kuongeza, 
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nasir
"kuna sheria gani ya kuwapiga Risasi waislamu msikitini, mimi pia ni mtungaji Sheria wa Bunge la Kenya, sijui wametumia Sheria gani ya kuwapiga Risasi watoto wenye umri wa miaka 12, na kama kuna sheria hiyo mimi nitakuwa radhi kung'oka kwa sababu siwezi kuwatumikia watu tunao wadhulumu, kuingia kwenye msikiti na kuweza kuwapiga risasi watu ndani ya msikiti hakuna sheria kama hiyo Kenya!". 

Alipoulizwa kuhusu hoja ya Polisi kuwa waislamu waliokuwa ndani ya Msikiti walikuwa na Silaha na kuhatarisha Usalama wa Taifa alisema, "kwanza mimi swali langu ni moja, Polisi wao wanasema Vijana wao walikuwa na silaha, kwanini wasingetumia busara kama vijana walikuwa na silaha maana wapo Maaskari waislamu wangeweza kutumika kuingia Msikitini kwa nidhamu na kuwaonya vijana kusalimisha silaha zao kwa utaratibu na bila kusababisha hasara na kuwaua watoto wasio na hatia".

Sikiliza mahojiano ya Mbunge huyo na msemaji wa Polisi