Friday, 7 February 2014

BALOZI WA MAREKANI NCHINI SUDAN ASILIMU, ALAZIMISHWA KUJIUZULU UBALOZI

Balozi mdogo wa Marekani nchini Sudani Joseph D Stafford amelazimishwa kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake mara baada ya kusilimu, vimeripoti vyombo vya habari vya ndani vya Sudan.

Stafford aliiambia wizara ya kigeni kwamba kujiuzulu kwake kumetokana na 'sababu binafsi'. Lakini vyanzo vya Sudan vilidai kuwa balozi huyo alilazimishwa kujiuzulu baada ya kubadili dini na kuwa muislamu.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa Stafford anakumbukwa kwa kufanya ziara katika makao makuu ya Ansar al- Sunnah nchini Sudan na kuanzisha uhusiano wa karibu na viongozi wa dini ambapo imepelekea kusilimu kwake.

Stafford baada ya kujiuzulu alichapisha makala katika Sudan Tribune na kusema, "Mimi na mke wangu tumekuwa na bahati sana ya kukutana na watu wengi wazuri (ajabu) katika Sudan ambao wana hamu kubwa na nia ya kuboresha jamii zao".

"Daima tutawakumbuka nyinyi na nchi yenu yenye kuvutia, najua mtaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya maisha bora kama msemavyo  'Fi Kulu Harakah Baraka' (katika kila haraka kuna baraka)".

Aliwahi kuwa Balozi katika nchi za Nigeria na Gambia. 
Miji aliyowahi kufanya kazi ni Baghdad (iraq), Abidjan (ivory coast),Tunis (Tunisia), Algiers (Algeria), na Nouakchott. kuwait,Cairo (Misri), Palermo (italy) na Tehran(Iran).

Stafford anayemudu lugha za kiarabu, kifaransa na kiitaliano alijiunga na wizara ya mambo ya nje ya marekani tangu mwaka 1978. Ana mke na mtoto mmoja.

Ubalozi wa Marekani mpaka sasa haujatoa kauli yoyote kuthibitisha au kukataa habari za Joseph Stafford.

pamoja na viongozi wa dini
katika hadhara ya dini
Akiitikia Dua
Joseph D Stafford