Shahin anayejulikana kama 'mhubiri wa mapinduzi' alisema kuwa huwezi kulala na mtu ambaye ni 'kidudumtu' katika chumba chako.
Akizungumza katika televisheni ya Misri alisema, "Kuna vitu vya kuvipa kipaumbele, je ni kipi cha kukitoa kati ya mke na nchi? Mke ni mtu na anaweza kuondoka. Lakini ninaposema kumuondosha simaanishi kumuua, Ninachomaanisha ni kumpa talaka na kumpa haki zake zote anazostahiki, nakumwambia mimi nalinda nchi yangu na uzalendo wangu".
Imamu Shahin ambaye aliwahi kusimamishwa katika msikiti mmoja kutokutoa mawaidha alisema msikiti huo ulimkataa kwa kuwa ni waungaji mkono wa Ikhwanul Muslimini.
"Wanachama wa chama hicho wamekuwa wakinilalamikia kuhusu mawaidha yangu yanasababisha mgawanyiko jambo hilo si kweli, mimi ninachohimiza ni umoja na mawaidha yangu yapo wazi sana", alisema Shahin.
Ikhwanul Muslimin kimepigwa marufuku nchini Misri kufanya harakati zozote na kimewekwa katika orodha ya vyama vya kigaidi nchini Misri.
![]() |
| Imamu Mazhar Shahin |
