Wednesday, 5 February 2014

RADIO SAUTI YA QURANI YACHANGIA MSIKITI WA NGARANAIBO

Wadau wa kipindi cha Busati kinachorushwa na Radio Sauti ya Qurani ya mjini Dar es Salaam wameuchangia msikiti wa wamasai wa kijiji cha Ngaranaibo kilichoko wilaya ya Longido mkoani Arusha.

Mchango huo ulikabidhiwa jana jioni katika studio za Radio hiyo na kupokelewa na Sheikh yusuf Kidago kwa niaba ya watu wa Msikiti wa Ngaraibo. Kiasi kilichochangwa ni Shilingi Laki Tano na elfu Ishirini (520,000/-). 

Lengo la mchango huo ni kununua umeme jua (Solar power) kwa ajili ya msikiti. Pesa hizo zimechangwa na wadau wapatao 80 wa kipindi hicho cha Busati ambapo pesa hizo zilikusanywa kwa muda siku tatu.

Kipindi cha Busati hurushwa siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa Kumi kamili alasiri hadi saa kumi na mbili za jioni, kikiendeshwa na watangazaji mahiri ustaadh Jamil Poli na Ukhti Tabu bint Salum.

Katika msafara wa kupokea kiasi hicho kilichochangwa Sheikh Yusuf Kidago aliambatana na Kiongozi wa kimila wa kimasai wa kijiji cha Ngaranaibo, Leigwanani Elinuru pamoja na Ustaadh Rashid Abubakar wa Namanga.

Mtangazaji Jamil Poli ndiye aliyemkabidhi Sheikh Yusuf Pesa ambapo naye baadae alimkabidhi Leigwanani Lenuru Nyikini.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mchango huo Sheikh Yusuf aliwashukuru wadau wa kipindi cha Busati, Watangazaji wake pamoja na Radio Sauti ya Qurani kwa moyo waliouonesha wa kuwasaidia waislamu wa Ngaranaibo.

Kijiji cha Ngaranaibo kinachokaliwa na jamii ya kimasai kimeanza kupata Nuru kwa watu wake kusilimu kwa wingi kuingia dini ya kiislamu.


Sheikh Yusuf Akimkabidhi bahasha yenye Pesa Leigwanani Lenuru Nyikini,
 nje ya ofisi za redio Sauti ya Qurani
Bahasha yenye Pesa