Wednesday, 5 February 2014

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA NORTH CAROLINA WADAI SEHEMU YA KUSALIA

Wanafunzi wa chuo kikuu cha North Carolina (North Carolina University) kilichopo Charlotte wameutaka uongozi wa chuo hicho kuwatengea eneo maalum kwa ajili kutekeleza ibada ya sala tano wawapo chuoni hapo.

"Kwa kukosa sehemu maalumu ya kusalia kuna wakati mtu unalazimika kusali katika ukumbi ambapo watu wanapita, imekuwa ni vigumu kupata nafasi ya kusalia", alisema Keyona Shears, 22 ambaye ni kiongozi wa mahusiano ya umma wa wanafunzi chuoni hapo kuliambia gazeti la Charlotte Observer.

Wanafunzi wa kiislamu chuoni hapo wamekuwa wakitumia vyumba vya madarasa tofauti tofauti kwa ajili ya kusali.
Imewalazima kila wakati wa sala kuingia ktafuta darasa ambalo lipo tupu na kuanza kufanya ibada.

Akizungumzia kadhia hiyo rais wa wanafunzi wa kiislamu chuoni hapo Mohamad Konsouh  alisema jambo lao wamelipeleka katika uongozi wa chuo na linafanyiwa kazi.

"Wakati wa siku ya ijumaa tumekuwa tunasali katika maktaba ya chuo ambapo si mahala pasafi sana lakini hakuna namna isipokuwa kutekeleza ibada yetu", alisema Konsouh.

Kwa mujibu wa Mohamad Konsouh wanafunzi wa kiislamu chuo hapo wanakadiriwa kufikia 1500.


wanafunzi wa kiislamu wakiwa mbele ya chuo