Ripoti iliyotolewa na Mahammat Saleh Annadif imeeleza kuwa, majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AMISOM yakishirikiana na majeshi ya serikali ya nchi hiyo yataendeleza operesheni za kijeshi kwa lengo la kuwatokomeza wanamgambo wa Al Shabab katika maeneo yote yanayoendelea kukaliwa na kundi hilo.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa, vikosi vya serikali vikishiriana na vile vya AMISOM hivi karibuni vilifanikiwa kuukomboa mji wa Hagar ulioko kusini mwa Somalia, baada ya kutokea mapigano makali yaliyopelekea makumi ya wanamgambo wa Al Shabab kuuawa na wengine kujeruhiwa.
Annadif ameongeza kuwa, vikosi hivyo pia vimefanikiwa kuukomboa mji wa Gandershe ulioko kati ya Mogadishu na Marka makao ya jimbo la Shabelle.
![]() |
| Mahammat Saleh Annadif |
