Monday, 10 February 2014

MBUNGE AUAWA HUKO JAMHURI YA AFRIKA YA KATI KWA KUWATETEA WAISLAMU

Jean- Emmanuel Ndjaroua Mbunge wa Bunge la mpito la Jamhuri ya Afrika ya Kati aliuawa jana huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana. 

Taasisi ya Muungano wa Haki za Binadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa, mbunge huyo aliuawa jana mara baada ya kumaliza kuzungumza na vyombo vya habari, ambapo katika hotuba yake alikosoa vikali kuendelezwa  wimbi la vitendo vya mauaji na ukandamizaji vinavyofanywa dhidi ya Waislamu nchini humo.

Vitendo vya mauaji dhidi ya Waislamu vinaendelea kwa kasi nchini humo katika hali ambayo, majeshi kutoka nchi za Kiafrika  yakishirikiana na yale ya Ufaransa yako nchini humo kwa kisingizio cha eti kuzuia mauaji, vitendo vya uporaji na mapigano kati ya makundi hasimu katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, zaidi ya Waislamu laki nane wamelazimika kuyakimbia makazi yao wakihofia kushambuliwa na makundi ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka, ambao wanaendeleza mauaji dhidi ya Waislamu nchini humo.
Askari wa kifaransa