Friday, 21 February 2014

MSIKITI IRSHAAD WA NAMANGA WACHOMWA MOTO, WAUMINI WAWAHI KUZIMA

Msikiti wa Irshaad wa mjini Namanga uliopo wilaya Longido Mkoani Arusha jana umenusurika kuchomwa moto na mtu asiyejulikana.

Mashuhuda wa tukio walisema mtu huyo ambaye hakutambulika vizuri aliingia aliingia msikiti hapo majira ya saa nmwane asubuhi kwa kupitia sehemu ya wanawake.

Inasemwa alipofanikiwa kuingia alimwagia mafuta ya taa zulia na kuliwasha kwa kibiriti. Moto mkubwa ulianza kushika kasi ndipo watu walipofika msikitini hapo kuona nini kinaendelea.

Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuwahi kuuzima moto kabla haujaleta madhara makubwa na hasara. Sehemu zilizoathiriwa na moto huo ni Dari, Zulia, pamoja na kuta kadhaa za msikiti huo. 

Mtu aliyesababisha moto huo alifanikiwa kutoroka na hakuweza kubainika mara moja. Aidha ilikutwa chupa
yenye mafuta ya taa na kibiriti. Baadae polisi walifika eneo la tukio na kuahidi kuanza upelelezi mara moja kutambua mtu aliyehusika na tukio hilo.

Bado haijafamika hasara iliyopatikana kutokana na uharibifu huo.


Kuta ikiwa imeharibiwa na moto
sehemu ya juu ya paa
Chupa yenye mafuta ya taa, iliyosahaulika
Busati zilizoungua,pamoja ceiling board

masjid Irshaad
masjid Irshaad