Mabuldoza yamewekwa tayari kubomoa jengo lililoko katika mji mtakatifu wa Makka katika mahala panapo aminika kuwa ndipo alipozaliwa Mtume ﷺ.
Ubomoaji wa jengo lijulikanalo kama Nyumba ya Mawlid, ni sehemu ya mradi wa mabilioni ya dola wa kujenga jengo kubwa la kisasa karibu na Masjidul Haram, eneo takatifu zaidi la Kiislamu na mahala ilipo Al Kaaba, kibla cha Waislamu.
Kwa mujibu wa wanahistoria, jengo la mahala alipozaliwa Bwana Mtume Muhammad ﷺ ndilo eneo pekee la kihistoria lililosalia nchini Saudi Arabia.
Utawala wa kifalme wa Aal Saudi umeunga mkono mpango wa ustawi mpya kwa gharama za kufuta athari za majengo ya kale.
Mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita wa 2013 Mufti Mkuu wa Saudia Sheikh Abdul Aziz Bin Abdullah al-Sheikh alitetea mpango huo wa kubomoa turathi za zama za mwanzoni mwa Uislamu katika mji mtukufu wa Makka.
Kiongozi huyo mkuu wa kidini nchini Saudi Arabia alifika mbali zaidi hata kuelezea ubomoaji huo kuwa ni jambo la lazima.
| muonekano wake wa mbele |
| alipozaliwa Mtume |