Friday, 21 February 2014

ANT-BALAKA HAWATAKI WAISLAMU WARUDI KATIKA MAKAZI YAO

Afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa anasema ghasia za kidini zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya kati zinaonekana kuwa mbaya zaidi.

Katika taarifa ya Jumatano kamishna  anayehusika na maswala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay alisema ukiukwaji mwingi wa haki unaendelezwa na kundi la wanamgambo wanaojiita anti-balaka ambao amesema kwamba wanalenga kwa maksudi waislam katika mji mkuu Bangui.

Pillay amesema wanamgambo hao wanauwa na kuwabaka waislam na kuharibu nyumba zao na wana nia ya wazi ya kuwazuia waislam kurudi kwenye makazi yao.