Fujo hizo zilianza alasiri ya jana baada ya vijana kurushia mawe magari na kuchoma pikipiki kadhaa ikiwa ni muendelezo wa ghasia zilizoanza Jumapili, suala lililosababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara za mji huo.
Polisi ilianza kuwatawanya vijana hao kwa kufyatua risasi na kutumia gesi ya kutoa machozi ambapo mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kutiwa mbaroni.
Machafuko hayo yalianza Jumapili baada ya polisi ya Kenya kuvamia msikiti wa Mussa mjini Mombasa na kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja mkusanyiko wa vijana wa Kiislamu ambapo watu watano waliuawa na mamia ya wengine kutiwa mbaroni. Polisi ya Kenya imedai kuwa, vijana waliokuwa kwenye msikiti huo walikuwa na silaha.
![]() |
| vurugu za jumapili |
