Tuesday, 18 February 2014

KUNDI LA ANSAR BEIT AL MAQDIS LADAI KUHUSIKA NA SHAMBULIZI LA BASI LA WA ATALII MISRI

Kundi la Ansar Beit al-Maqdis la eneo la Sinai, lenye mahusiano na kundi la Al-Qaeda limedai kuhusika na shambulizi la bomu dhidi ya basi lililokuwa limebeba watalii kutoka Korea Kusini, lililotokea jana katika peninsula ya Sinai na kusababisha vifo vya watu wanne. 

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa internet na kundi hilo imesema kundi hilo linahusika na shambulizi dhidi ya basi la watalii la Taba. 

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya wakorea watatu na mmsiri mmoja, na wakorea wengine 13 na wamisri wanne walijeruhiwa. 

Taarifa hiyo pia imesema kundi hilo litaendelea kuwalenga viongozi wa nchi na uchumi wa Misri, kwa kushambulia sekta ya utalii na kulipua mabomba ya gesi.

Basi lililolipuliwa na bomu