Rais wa Marekani Barack Obama amemuonya Rais wa Uganda Yoweri Museveni dhidi ya kuidhinisha sheria inayoharamisha ushoga, na kutaja hatua hiyo kwamba itaathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Obama aliyekuwa California kwa mapumziko ya wikiendi alitoa taarifa kali iliyosema amehuzunishwa sana na mpango wa kiongozi wa Uganda wa kutaka kutekeleza mswada huo.
“Tunaamini kwamba watu kila mahali wanafaa kuhudumiwa kwa usawa, kwa heshima na kuwa wanafaa kuwa na nafasi ya kutumia uwezo wao kikamilifu, bila kujali wao ni kina nani au wanaowapenda,” ilisema taarifa hiyo.
Ameeleza kwamba mswada huo ni wa kidhalimu na hatari kwa jamii ya mashoga nchini Uganda.
Ameeleza kwamba mswada huo ni wa kidhalimu na hatari kwa jamii ya mashoga nchini Uganda.
“Hiyo ndiyo maana nimeudhika sana kuwa Uganda itaidhinisha sheria ambayo itaharamisha ushoga hivi karibuni,” iliendelea taarifa hiyo.
taarifa inafafanua zaidi kwamba, “Mswada unaopinga ushoga Uganda utakapokuwa sheria, itakuwa ni kushambulia na kufanya iwe hatari kwa jamii ya mashoga Uganda. Itakuwa ni hatua ya kurudi nyuma kwa wananchi wote wa Uganda na itatoa sifa mbaya kwa Uganda kujitolea kulinda haki za kibinadamu za wananchi wake.”
Sheria hiyo ilipitishwa na wabunge wa Uganda mnamo Desemba mwaka jana baada ya wale walioinakili kuondoa sehemu iliyopendekeza hukumu ya kifo.
Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela.
Hatua hiyo ambayo imeibua malalamishi makali kimataifa, itaharamisha utangazaji au utambuzi wa uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja.

Obama alisema kuwa rais wa Uganda, ambaye ni kiongozi muhimu kutoka Afrika kwa utawala wa Marekani na Muungano wa Ulaya, huenda akapelekea kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya nchi yake na Marekani ikiwa ataidhinisha mswada huo kuwa sheria.
“Tumemwambia Rais Museveni kuwa uidhinishaji wa sheria hiyo utatatiza uhusiano muhimu uliopo kati yetu na Uganda,” alisema Obama.
Mshauri wa Obama kuhusu usalama wa kitaifa Susan Rice aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kuwa uidhinishaji wa sheria hiyo utahatarisha maisha ya wengi na kuharibu sifa ya Uganda.
Aliongeza kuwa alijadiliana kwa kina na Rais Museveni kumwomba asiidhinishe mswada huo jumamosi usiku.
Museveni, awali alitoa maoni yake kuwa mashoga ni wagonjwa na wana matatizo.
Alieleza kwenye barua aliyowasilisha kwa bunge kuwa ushoga husababishwa na matatizo ya kimaumbile, au hitaji la kujipatia pesa. Hata hivyo, alikataa kuidhinisha sharia hiyo mwezi uliopita.
“Hapendi ushoga lakini anaamini kuwa watu hao wana haki ya kuishi,” msemaji wa rais Tamale Mirudi aliambia AFP wakati huo, na kueleza kwa nini mswada ulikataliwa na rais.
Idadi kubwa ya raia wa Uganda huchukizwa na ushoga. Watu walio na uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja huhangaishwa mara kwa mara huku wakipokea vitisho.
Ushoga ni jambo linalotiliwa mkazo na watu wa Ulaya na Amerika kuzisisitiza nchi za Afrika kutambua haki za jamii hiyo kwa vitisho vya kutopewa msaada pindi zisipotambua haki zao.
Ni muhimu sasa jamii ya kiislamu kuimarisha zaidi madrasa kwa ajili ya kuwajenga vijana katika misingi ya dini ili kuwa kuwaepusha na wimbi linalokuja kwa kasi la ushoga.
Ni muhimu sasa jamii ya kiislamu kuimarisha zaidi madrasa kwa ajili ya kuwajenga vijana katika misingi ya dini ili kuwa kuwaepusha na wimbi linalokuja kwa kasi la ushoga.
![]() |
| Barack Hussein Obama |