Mkuu wa vikosi vya usalama vya Serikali ya Mpito ya Jubba (IJA), Issa Mohamed Alaaki, anayefahamika pia kama Issa Kamboni, aliuawa usiku wa Jumatatu mjini Kismayo na mlinzi wake anayeripotiwa kuwa mwanachama wa zamani wa al-Shabaab.
Walinzi wa usalama wa IJA walifika kwenye eneo la tukio haraka na kukuta miili ya watu watatu waliopigwa risasi, liliripoti gazeti la Dhanaan Media la Somalia
Muuaji alimpiga Alaaki risasi akiwa ndani ya gari yake pamoja na walinzi wengine wawili na kisha kukimbia. Operesheni ya msako ilifanywa mjini Kismayu kumtafuta.
Mtuhumiwa huyo anaripotiwa kuliasi kundi la al-Shabaab miezi michache iliyopita na kujiunga na vikosi vya usalama vya IJA. Pia anaaminika kuwa jamaa wa karibu na Alaaki.
