"Hizo ni harakati zisizokubalika na zinaweza kuongeza hali hiyo kwa kuwaudhi vijana zaidi na kuimarisha hisia miongoni mwao kwamba serikali iko kinyume nao, hivyo kuwafanya kuwa na siasa kali zaidi," mjumbe wa kamati ya msikiti wa Jamia wa Nairobi Ibrahim Lethome alisema.
"Mpango wa serikali utafanya Waislamu kuona vita vyote hivyo dhidi ya ugaidi kama vinavyolenga isivyo haki Waislamu ambako kutazuia ushirikiano baina ya jamii na serikali", alisema.
Lethome alisema kufungwa kwa misikiti ni ukiukwaji wa uhuru wa kusali na kunaweza kuonekana kama kutoa adhabu ya jumla kwa jamii yote ya Waislamu.
Kuepuka vitendo vya ghasia zaidi katika misikiti, Lethome alishauri serikali kutumia upelelezi kubaini kabla matukio yoyote ya uhalifu au shughuli zinazohusiana na ugaidi katika maeneo ya swala.
Kamishina wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa ametishia kufunga misikiti miwili katika jiji hilo Masjid Mussa na Masjid Sakina kufuatia mapigano baina ya polisi na vijana wa Kiislamu wiki iliyopita.Kuepuka vitendo vya ghasia zaidi katika misikiti, Lethome alishauri serikali kutumia upelelezi kubaini kabla matukio yoyote ya uhalifu au shughuli zinazohusiana na ugaidi katika maeneo ya swala.
| Kamishina wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa |