Wednesday, 12 February 2014

KAMPUNI YA INTERNET YA HORMUUD TELECOM YAFUNGA HUDUMA ZAKE SOMALIA KWA SHINIKIZO LA AL SHABAB

Kampuni ya simu ya Hormuud Telecom siku ya Alhamisi imezima huduma za intaneti kwenye simu za mkononi mjini Mogadishu baada ya kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa wanagambo wa Al Shabaab walioziamuru kampuni za simu kuacha kutoa huduma ya intaneti mwezi uliopita.

Hatua hiyo ya Hormuud kufunga huduma za intaneti kwenye simu za mikononi mjini Mogadishu imekuja chini ya wiki moja baada ya Al Shabaab kuwakamata wafanyakazi 16 wa kampuni hiyo katika mji wa Jilib mkoani Jubba ya Kati, akiwemo meneja wa tawi, Mohamud Haji Salad.

Hata hivyo, wanamgambo hao wameripotiwa kuruhusu kurudi kwa huduma ya intaneti kwenye simu za mikononi katika mikoa ya Jubba ya Kati na Chini siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa Redio RBC.


Kampuni ya simu ya Hormuud Telecom