Thursday, 13 February 2014

33 WALIOKAMATWA KATIKA VURUGU ZA MASJID MUSSA WAACHIWA HURU

Serikali ya Kenya siku ya Jumanne (tarehe 11 Februari) iliwaachia washukiwa 33 waliokamatwa wakati wa uvamizi wa Masjid Mussa huko Mombasa mapema mwezi huu, na kushikiliwa kwa unyang'anyi na vurugu dhidi yao, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.

Washukiwa waliokamatwa wanatakiwa kuripoti katika Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (CID) kila Jumatano. Serikali pia inalinda haki ya kuwakamata tena na kuwahoji kulingana na matokeo ya uchunguzi unaoendelea.

Walioachiwa huru ni pamoja na wanawake watatu na vijana wa kiume wenye umri chini ya miaka 20 au zaidi kidogo. Washukiwa sabini na moja bado wapo chini ya uangalizi wa polisi.

Kompyuta za laptop, nyaraka na vifaa vingine vilivyokamatwa katika  uvamizi wa tarehe 2 Februari bado viko katika kitengo cha kuzuia uhalifu cha CID kwa ajili ya uchunguzi.