Thursday, 13 February 2014

IMAMU AGOMA KUONDOKA BANGUI, ASEMA ATAKUWA MUISLAMU WA MWISHO KUONDOKA AU KUFA

Imamu mmoja wa msikiti mjini Bangui amesema kwamba hafikirii kuondoka wala kikimbia mji huo licha ya mashumbilizi na mauaji dhidi ya waislamu kutoka kwa wanamgambo wa kikristo wa Ant balaka. 

"Sitaki kuondoka Bangui, nataka kuwa wa muislamu wa mwisho wa Afrika ya Kati kuondoka nchini au kuwa muislamu wa mwisho kuuliwa na kuzikwa hapa," Imam wa huyo wa Bangui aliiambia BBC katika kipindi cha Newsday.

Aliongeza kusema kuwa, "Hii nchi ni mahala alipozikwa baba yangu na mama yangu. Ant Balaka wamekuwa wakitulenga sisi, Wameweza kuchoma moto misikiti mingi zaidi katika mji mkuu, na michache tu ndio imebaki bila kuguswa katika kitongoji chetu", alielezea. 

Imam aliongeza, "Kama wanataka kutuua na iwe hivyo, hatuna silaha, lakini tupo tayari kukubali hatima yetu kwa sababu tunaamini katika Mungu na tuna hakika kwamba Mungu atatulinda", alimaliza.

Vitendo vya mauaji dhidi ya Waislamu vinaendelea kwa kasi nchini humo katika hali ambayo, majeshi kutoka nchi za Kiafrika  yakishirikiana na yale ya Ufaransa yako nchini humo kwa kisingizio cha eti kuzuia mauaji.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, zaidi ya Waislamu laki nane wamelazimika kuyakimbia makazi yao wakihofia kushambuliwa na makundi ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka, ambao wanaendeleza mauaji dhidi ya Waislamu nchini humo.


Mmoja wa wazee wa kiislamu