Taarifa zinasema mapigano yalikuwa makali baada ya waumini wa kipalestina kusimama na kuanza kujibu mapigo ya vikosi vya Israel.
Mapigano hayo yalizuka baada ya vikosi vya Israel kuvamia eneo hilo na kuanza kurusha mabomu ya mchozi na risasi za mpira.
Mlinzi wa msikiti huo Othman Abu Ghyarbiyeh alisema vikosi vya Israel vilifunga geti la Al Qibali na kupulizia gesi yenye pilipili kwa waumini wakipalestina.
"Watoto watatu, wanawake wawili na wanaume kumi walijeruhiwa wakati wa mapigano," alisema Abu Ghyarbiyeh .
Msikiti wa al Aqswa uliopo katika mji wa al Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel umekuwa kitovu cha vurugu na machafuko.
Mayahudi wanataka kubomoa msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu kwa kisingizio cha kutafuta mabaki ya hekalu la Nabii Sulaiman.
Aidha taarifa zinasema Israel imepanga kubadilisha sura ya sehemu ya msikiti huo ya al Buraq na vilevile kujenga njia ya mabasi yaendayo kwa kasi katika eneo la kati ya Jabalu-turi na Babul-asbat, na kueleza kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa lengo la kuyayahudisha maeneo matakatifu na kufuta athari za Kiislamu.
Taarifa zinasema israel imeashiria mpango wa kujenga hekalu katika eneo la sehemu moja ya tano ya msikiti wa Alqsa. Msikiti huo mtukufu ni milki ya Waislamu wote duniani.
