Thursday, 27 February 2014

ANT-BALAKA WAENDELEA KUBOMOA MISIKITI NA KUUA WAISLAMU

Kundi la Kikristo la Anti Balaka linaendeleza jinai dhidi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kubomoa makumi ya Misikiti nchini humo. 

Taarifa zinasema kuwa, kundi la Anti Balaka linafanya mikakati ya kufuta athari zote za dini tukufu ya Kiislamu na Waislamu kwa kuwauwa Waislamu na kubomoa Misikiti yao. 

Taarifa hizo zimeongeza kuwa, mji mkuu wa jamhuri ya Afrika ya Kati umbao ulikuwa na Misikiti 36, hivi sasa umesalia na misikiti chini ya kumi tu, baada ya makumi ya mingine kubomolewa na wanamgabo wa Kikristo wa Anti Balaka.

Wakati wanamgambo wa Anti Balaka wakiendeleza jinai zao za kuwauwa kinyama Waislamu hata walioko ndani ya Misitkiti katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, vikosi vya askari wa kimataifa vya kulinda amani vimeshindwa kulinda maisha ya Waislamu nchini humo.

Hivi karibuni, gazeti la Daily Telegraph la Uingereza lilitangaza kuwa, genge la Anti Balaka limekuwa likifanya mauaji kwa kuwakatakata kwa mapanga, kuwatesa, kuwachoma moto na hata kuwapiga risasi Waislamu, huku vikosi vya kulinda amani vikishindwa kuzuia jinai hizo.

Ant-Balaka