“Unaweza kubadili mtazamo kuhusu sheria hii kwa weusi au wayahudi na unaweza kuona miaka ya 30 nchini Ujerumani au miaka ya 50 na 60 kulipokuwa na ubaguzi Afrika Kusini,” alisema akihutubia kikundi kidogo cha wanahabari.
Siku ya Jumatatu, rais Yoweri Museveni wa Uganda alitia saini mswada ambao ni sheria inayowafunga jela maisha watu wanaopatikana kwa mara ya pili na hatia ya kushiriki ushoga.
Sheria hiyo pia inapiga marufuku vitendo vya kupigia debe ushoga na inawataka watu wawakane na kuwatenga mashoga na wasagaji.
“Kilichotokea Uganda ni uhaini na kitatupatia sote changamoto kubwa, kwa sababu wasagaji, mashoga, watu wenye jinsia mbili na wengine wana haki za kimsingi kama binadamu wengine. Kutia saini sheria ya kukataza uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja ni makosa kimaadili,” alisema.
“Kama ambavyo ilikuwa makosa kwa Wajerumani wa utawala wa nazi kuangamiza Wayahudi na makaburu walivyoendeleza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, kitendo cha kupitisha sheria hii ni makosa vile vile,” aliongeza.
Bw Kerry alionya kwamba ubaguzi dhidi ya mashoga ni 'mkubwa zaidi kuliko ulivyo Uganda' na kwmaba mataifa 78 ulimwenguni yana sheria ambazo 'zinakiuka haki za kinsingi za binadamu hao'.
![]() |
| John Kerry |
