Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughuliwa masuala ya kibinadamu nchini Myanmar ametaka kukomeshwe mauaji dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya katika mkoa wa Rakhine.
Tomas Ojea Quintana ametahadharisha kuwa, kufumbia macho ukatili wanaofanyiwa Waislamu wa Mynamar kunaweza kuhatarisha mipango ya mageuzi na demokrasia kwenye nchi hiyo.
Ripota huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar ameitaka serikali ya nchi hiyo kushughulikia machafuko yanayojiri kwenye mkoa wa Rakhine yanayowalenga Waislamu.
Maelfu ya Waislamu wa Myanmar wameuawa na wengine wengi kulazimika kukimbia makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali.
Serikali ya Myanmar imekuwa ikikosolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwa kushindwa kuwalinda Waislamu wa nchi hiyo ambao ni jamii ya wachache.