Waziri wa mambo ya ndani na uzalendo Pascal Barandagiye ametolea wito waumini wa dini ya kiislamu Jumanne kuwa na mke mmoja pekee ili kuheshimu sheria.
Kiongozi huyo alisema kuwa waumini wote wa kiislamu ambao wana wake zaidi ya mmoja wanaombwa kufunga ndoa kisheria na mwanamke mmoja pekee kabla ya mwaka 2017 kumalizika.
Pascal Barandagiye aliyazungumza hayo katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari mjini Bujumbura.
![]() |
Pascal Barandagive |
Akizungumzi kuhusu wanamume wenye wake zaidi ya mmoja wakidai kuruhusiwa na uislamu, Waziri Pascal amesema kuwa tayari walizungumza na wataalamu wa dini kuhusu suala hilo.
Waziri amesema kuwa wataalamu wa dini walifahamisha kuwa wanaume wanaoruhusiwa kuwa na mke zaidi ya mmoja ni wale wenye uwezo na kuwatendea haki sawa wake zao.
Burundi ni taifa lisilo kuwa la kidini na sheria hiyo inahusu raia wote nchini alizidi kufahamisha waziri.
Asilimia 10 ya raia nchini Burundi ndio waumini wa dini ya kiislamu wengi wao wakipatikana mijini kama Bujumbura, Gitega na Rumonge.
Uongozi wa kiislamu nchini Burundi COMIBU bado haujazungumza lolote kuhusu suala hilo.