Tuesday, 18 July 2017

MSIKITI WA AL AQSA WAENDELEA KUFUNGWA KWA SIKU MBILI MFULULIZO

Mamlaka nchini Israel imeendelea kufunga msikiti mtakatifu wa Al Aqsa tangu tukio la risasi dhidi ya wapalestina 5.
Serikali nchini Israel imepiga marufuku kufanyika ibada za sala na pia kuita adhana kutoka msikiti huo.
Aidha viongozi wa kidini wamenyimwa kutoa mafunzo katika Al Aqsa .

Mbali na kufunga msikiti huo wamemtia kizuizini mufti mkuu wa Jerusalem, Sheikh Muhammad Huseyn kufuatia shambulio hilo.