Thursday, 6 July 2017

RIPOTI: MILO YA FUTARI MILIONI 30 ILITOLEWA KATIKA MSIKITI WA MAKKAH

Milo zaidi ya milioni 30 ya Futari ilitolewa kwa waumini ndani ya msikiti mtukufu wa Makkah na maeneo ya nje ya msikiti huo kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa kwa Gavana
Prince Khaled Al-Faisal.

Prince Khaled Al-Faisal alipokea ripoti hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa kamati kuu ya Hijja Hisham bin Abdulrahman Al-Faleh.
Vijana waliojitolea wakiwa Maji kwa Waumini
Pakiti za milo milioni 25.11 za futari ziligawanywa kwa waumini ndani ya msikiti na milo 5.11 milioni walipewa waumini nje ya msikiti katika maeneo ya umma kama vile mabasi ya abiria.

Prince Khaled alishukuru mashirika ya serikali na mashirika yasiyo ya serikali yaliyojitolea kuwahudumia mamilioni ya mahujaji msimu wa mwezi wa ramadhani.

Waumini wapatao milioni 3 watokao nje ya nchi na milioni 2 watokao ndani ya Saudi Arabia walizuru Msikiti wa Makkah kwa ajili ya Ibada ndani ya Ramadhani ya mwaka huu.

Mpango huo wa kimkakati ulitekelezwa na kamati inayojumuisha mashirika kama vile wizara ya mambo ya ndani, afya, masuala ya Kiislam, ulinzi wa kiraia na mashirika mengine ya sekta binafsi.