Saturday, 27 May 2017

RAMADHANI 2017: NCHI ZENEYE MASAA MENGI ZAIDI YA KUFUNGA

Waislamu kote dunia wameingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani huku baadhi ya sehemu wakitarajia kufunga masaa mengi zaidi na maeneo mengine kufunga masaa machache.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Ummid, nchi ya Iceland ndio inayoongoza kwa kuwa na masaa mengi ya kufunga kwa mwaka 2017.

Iceland watafunga kwa muda wa masaa 21, wakifuatiwa na Finland masaa 19:56, Norway masaa 19:48 na Sweden masaa 19:42. 

Masaa haya yamekadiriwa kutokana na kuingia kwa swala ya Alfajiri na Magharibi katika nchi hizo.

Nchi zingine za ulaya zitakazo kuwa na masaa mengi ya kufunga ni Russia masaa 19:07, Denmark masaa 19:05, Belarus masaa 18:52, Ujerumani  masaa 18:51, Ireland masaa 18:48 na United Kingdom masaa 18:34.

Katika Afrika nchi ambazo zitakuwa na masaa mengi ya kufunga ni Nigeria kwa masaa 13:50 na Zimbabwe kwa masaa 12:26.

Nchi ya Argentina na Australia ndizo zinazoonekana kuwa na masaa ya machache ya kufunga kwa kuwa na masaa 11:32.