Friday, 26 May 2017

MIAKA 3 JELA KWA KUMPIGA MATEKE YA TUMBO MJAMZITO KWA CHUKI YA KIDINI

Mwingereza aliyempiga teke la tumbo mwanamke mjamzito na kusababisha kuharibika kwa ujauzito wa mapacha amehukumiwa miaka mitatu na miezi saba jela.

David Gallacher alimshambulia Samsam Haji Ali 34, huko Buckinghamshire Septemba 2016.

Alimpiga teke hilo katika maegesho ya magari na kuanza kutokwa na damu iliyochuruzika mpaka kwenye sakafu na baada ya wiki chache ujauzito ukaharibika.

Aidha katika shambulio hilo lililotajwa kama la uvamizi wa kijambazi na ubaguzi wa kidini, Abdullah sulamain, 40, ambaye ni mume wa Samsam alishambuliwa kwa kupigwa na chupa ya wine.

Mwendesha mashitaka Christopher Wing mapema aliieleza mahakama kwamba Samsam alikuwa amekaa katika gari lake wakati Gallacher alipomkaribia na kuanza kumtupia
maneno ya kumkashifu. 
David Gallacher
Samsam aliposhuka na kuelekea katika duka, Gallacher alimfuata na kuanza kumpiga mateke ya tumbo licha ya kuambiwa mwanamke huyo ni mjamzito. 

Wakati anamrushia mateke hayo pia alikuwa akimtolea maneno ya ubaguzi unaoashiria chuki ya kidini.

Gallacher alikiri makosa mawili ya kibaguzi na kushambulia kulikosababisha madhara ya mwili na kosa tatu kumshambulia afisa wa polisi.