Bunge la Ugiriki limeupitisha muswada unaoruhusu kujengwa kwa msikiti wa kwanza mjini Athens.
Chama cha mrengo wa kulia Golden Dawn and Independent Greeks (ANEL) pekee ndio kilipiga kura ya hapana dhidi ya kupitishwa kwa muswada huo.
Msikiti wenye uwezo wa kubeba watu 350 unajengwa katika mji mkuu wa Votanikos nchini Ugiriki.
Msikiti huo utakuwa ni wa kwanza mjini Athens na wa kwanza kujengwa kwa kutumia leseni ya taifa la Ugiriki toka karne ya 19.
Naibu waziri wa mambo ya nje ameupongeza sana muswada huo.
Anaamini kuwa Ugiriki imefanya jambo la maana sana kuupigia kura muswada huo kwani ni heshima kubwa kwa haki za binadamu na utasaidia kudumisha umoja na amani nchini humo.
Bunge liliruhusu ujenzi huo kuendelea mwezi Agosti mwaka jana kabla ya chama cha mrengo wa kulia kuingilia kati.
Hata hivyo ujenzi huo unatarajia kumalizika mwezi Julai.
Athens ndio mji mkuu pekee ulaya ambao haukuwa na msikiti.