Katika video iliyosambaa katika mitandao ya Intaneti, Ustaadh Ja'afar Abdul Rahman alikuwa anasoma aya ya pili ya Suratul Al Mulk katika mji wa Surabaya Indonesia siku ya Jumatatu wakati sauti yake ilipoanza kufifia kabla ya kuzimia.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Indonesia, Ustaadh Ja'afar aliaga dunia dakika chache baada ya kuzimia.
msomaji huyo alikuwa akisoma Qur'ani katika kikao kilichokuwa kimehudhuriwa pia na Waziri wa Masuala ya Kijamii Indonesia Khofifah Indar Parawansa.
Madaktari wanasema alipata mshtuko wa moyo na hivyo kushindwa kumaliza Qiraa hicho.
Ustadh Ja'afar alikuwa msomi mashuhuri wa kidini Indonesia na alikuwa anawavutia wengi kwa Qiraa chake kizuri na maridadi cha Qur'ani Tukufu.
Sehemu ya Qurani aliyosoma na kushindwa kuendelea na kufariki ni,
........ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ
الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا
Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.....
Ambaye ameumba mauti na uhai kukujaribuni