Friday, 28 April 2017

BUNGE UJERUMANI LAPITISHA MARUFUKU YA KUVAA NIQABU

Siku ya Alhamis bunge la Bundestag la Ujerumani lilipitisha marufuku ya vazi la Niqabu linalovaliwa na waislamu.
Raia wa kawaida na wafanyakazi wa umma hawatoruhusiwa kuwa mitaani au sehemu za kazi wakiwa wamevalia vazi hilo la Niqabu.

Hatua hiyo imetolewa baada ya kansela wa Ujerumani Angela Merkel kutoa wito kupigwa marufuku vazi la kujifunika uso kwa waislamu mnamo Desemba mwaka jana .

Ujerumani si nchi ya kwanza kuweka marufuku vazi hilo hivi karibuni serikali za Austria pia ililipitisha marufuku hiyo dhidi ya waislamu .