Wednesday, 3 May 2017

MAANDAMANO KUPINGA CHUKI DHIDI YA UISLAMU YAFANYIKA AUSTRALIA

Raia wa Uturuki wanaoishi nchini Australia wamefanya maandamano ya amani ya kupinga matendo ya chuki dhidi ya waislamu nchini humo.
Vitendo vya chuki dhidi ya waislamu nchini Australia vimeongezeka katika siku za nyuma nchini humo.

Raia wa Uturuki waishio nchini Australia  wameandaa tamasha ambalo  wamelipa kaulimbiu «Yes We are Muslim» kwa kufungua  vibanda vidongo katika  barabara za Melburne na Sydney.

Hafla hiyo imeandaliwa kwa niaba ya  kukemea vitendo vinavyoaashiria chuki dhidi ya uislamu.

Katika hafla hiyo waandamanaji walitoa maua kwa wapita njia kuonesha ishara ya mapenzi na amani.