Wanawake wapiganaji ndondi wameruhusiwa kuvaa vazi la hijabu katika mchezo huo nchini Uturuki.
Chama cha ndondi duniani(AIBA) kimeruhusu vazi la hijabu wakati wa kupigana ndondi ndani ya Uturuki.
Kwa mujibu wa habari, Uturuki ilituma ombi hilo AIBA toka mwezi Februari.
Wanawake sasa hawatahitajika kuvua hijabu zao wakati wala baada mchezo huo.
Uamuzi huo umefuatiwa kuruhusiwa kwa mchezaji ndondi maarufu kutoka Minnesota kuvaa hijabu wakati wa ndondi nchini Marekani.
Vilevile mwanachama mtendaji wa AIBA nchini Uturuki amesema kuwa atatuma ombi jingine la sheria hio kuruhusiwa nchi zote.