Sunday, 23 April 2017

AMAIYA ZAFAR: BONDIA WA KIKE ALIYERUHUSIWA KUVAA HIJABU ULINGONI

Mwanandondi kijana wa kike na pia mwislamu kutoka Minnesota Marekani afanikiwa katika kupata ruhusa ya kuvaa hijab wakati wa mechi nchini Marekani.
Amaiya Zafar ameruhusiwa pia kujifunika katika mikono yake na miguu kulingana na masharti ya dini ya kiislamu kuhusu kujifunika kwa wanawake.

Amaiya mwenye umri wa miaka 16 hakuruhusiwa kushiriki mechi moja Florida na viongozi wa ndondi kwa kuwa alikuwa amevalia hijab,kujifunika miguu na mikono.

Amaiya ana ndoto ya kuweza kushiriki mechi za kimataifa hasa Olimpiki za mwaka 2020 jijini Tokyo.