Msichana mwenye umri wa miaka 17 ameshambuliwa kwa kuvaa hijabu mjini Berlin nchini Ujerumani.
Kwa mara nyingine nchini Ujerumani kunashuhudiwa kitendo cha unyanyasaji na ubaguzi baada ya mschana mwenye umri wa miaka 17 kushambuliwa kwa kuwa alikuwa kavaa hijabu.
Kitendo hicho kimetambulika kuwa kitendo cha ubaguzi na chuki dhidi ya waislmau nchini Ujerumani.
Watu waliomshambulia mschana huyo bado hawajatambulika.
Mschana huyo ameshambuliwa na watu watatu akiwemo mwanamke mmoja katika barabara ya Tempelhofer Damm.
Mschana huyo amejeruhiwa mkononi na kupelekwa hospitali kupewa matibabu.