Friday, 8 December 2017

QURANI YA ZAMA ZA UTAWALA OTTOMAN YAONEKANA MSIKITI WA PALESTINA

Quran tukufu tatu zilizochapishwa wakati wa utawala wa Otoman wa uongozi wa Sultan Abdul Hamid(1876-1908) zimepatikana katika msikiti wa Omar bin al-Khattab ulioko katika mji wa kale wa Tayibe nchini Palestina.
Quran hizo tatu zimepatikana kati ya vitabu vingine vya zamani wakati wa ukarabati wa msikiti huo.

Quran hizo zinaonesha jina la mwandishi kuwa aliyeandika kwa mkono ni Seyyid Mustafa Nazif na baadae kupelekwa na kuchapishwa Istanbul kabla ya kusafirishwa Palestina kwa ajili ya kuuzwa.

Muadhini wa msikiti huo Ustaadh Aziz alisema jumatatu wakiwa katika usimamizi wa ukarabati wa msikiti huo wakiwa wamekaa katika rundo la vitabu vingi ndipo walipoona
Qurani hizo za kale. 

Quran hizo zimeongeza historia ya msikiti huo na mji mzima kwa ujumla.