Thursday, 17 August 2017

MAHUJAJI WA QATAR RUKSA KUHUDHURIA HIJJA SAUDI ARABIA

Saudi Arabia itafungua mpaka wake na Qatar kuruhusu mahujaji kuhudhuria Hijja ya kila mwaka mjini Mecca kuanzia mwezi ujao, vyombo vya habari vinasema.

Tangazo hilo linakuja baada ya mkutano mkuu wa kwanza kati ya nchi hizo majirani, tangu Saudi Arabia na nchi zingine tatu kukata uhusiano na Qatar mwezi Juni.
Nchi hizo zinailaumu Qatar kwa kusaidia magaidi madai ambayo Qatar inayakana.

Kufungwa kwa mpaka wa Saudia kumeilazimu Qatar kuingiza chakula kupitia baharini na hewani kuweza kulisha watu wake milioni 2.7.

Mahujaji wa Qatar wanaotaka kuhudhuria Hijja watapitia eneo la Salwa bila kuhitaji vifaa vya eletroniki huku wengine wakiruhusiwa kupitia viwanja vya ndege vya Saudi Arabia.

Mwezi uliopita Saudi Arabia ilionya mahujaji wa Qatar kuwa wangekumbwa na vikwazo kadhaa ikiwa wangehitaji kuhudhuria Hija Qatar ilijibu kwa kuishutumu Saudia kwa kuligeuza suala la Hijja kuwa la kisiasa.

Lakini Saudia ilibadili msimamo huo baada ya mkutano kati ya mfalme ya Saudia Mohammed Bin Salman Al Saud na wa Qatar Abdullah bin Ali bin Abdullah bin Jassim Al Thani.