Jarida la serikali la Saudia Arabia limetangaza kuwa mahujaji 31 wameripotiwa kufariki Jumapili .
Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu sababu zilizopelekea maafa hayo.
Jarida hilo la "Saudi Press Agency" limesema kuwa watu waliofariki ni raia wa kigeni.
Mahujaji zaidi ya 620,000 wameshawasili nchini Saudia Arabia Agosti 12 kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hijja.
