Mwanamke raia wa Uturuki ambaye amehifadhi nusu ya Qur'ani hivi sasa anataraji kuhifadhi Qur'ani yote juzuu 30.
Bi Firuz Suntur ambaye anaishi katika mji wa Van mashariki mwa Uturuki alianza masomo ya Qur'ani hivi karibuni na si tu kuwa alifanikiwa kuweza kusoma kwa usahihi bali pia alihifadhi juzuu 15 za Qur'ani Tukufu.
Anasema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuhifadhi Qur'ani kutokana na matatizo ya kimaisha na kukosa wakati.
Anasema baada ya watoto wake wote kufanikiwa kuolewa sasa amepata muda wa kutosha kufanikisha lengo lake la muda mrefu.
Bi. Firuz mwenye umri wa miaka 69 anasema baadhi ya jamaa zake walikuwa wanaamini kuwa kwa umri wake hawezi kuhifadhi Qur'ani lakini anasema aliwapuuza na kusonga mbele na azma yake ya kuhifadhi Qur'ani.
"Nataraji kuwa siku moja nitaweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu," anasema.
Bi. Firuzi ni thibitisho wa kuwa na nia na azma, mwanadamu anaweza kufikia malengo matukufu na mafanikio hayo hasa hupatikana kwa kutowasikiliza wenye kutoa matamshi yenye kuvunja moyo.
Nini maoni yako juu ya habari hii, je nawe umepata hamasa ya kujifunza na kuhifadhi Qurani?
